"Kuhakikisha kuna utulivu wa bei na mfumo wa fedha wenye uadilifu kwa ukuaji jumuishi wa uchumi wa Taifa
"
"
Kuwa na uchumi imara, mfumo wa kisasa wa fedha na ongezeko la huduma jumuishi za fedha kwa ukuaji jumuishi wa uchumi wa viwanda Tanzania
"
Tunu za Benki zinaonesha namna tunavyotekeleza majukumu yetu na kushirikiana na wadau wetu. Kwa hiyo,kwa wakati wote tunaongozwa na tunu zifuatazo:
Uadilifu:
Tunatekeleza majukumu yetu kwa uadilifu unaojionesha katika uaminifu, utii, ukweli na usiri;
Ushirikishwaji:
Tunaamini katika ushiriki mpana, utendaji kazi wa pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu ili kufikia malengo yetu.
Ubora:
Tunatimiza wajibu wetu kwa umahiri na ubunifu ili kuendelea kuboresha utendaji wetu.
Uwajibikaji:
Kila mmoja na kwa umoja wetu tunawajibika kwa tunayoyafanya katika kutimiza matarajio ya wadau wetu.