Takwimu toka wa wasimamizi wa sekta ya fedha
  1. Taarifa ya ukaribu wa huduma za kifedha kwa watumiaji

    Taarifa ya ukaribu wa huduma za kifedha kwa watumiaji huonyesha ukaribu wa watu na biashara ndogo na za Kati (MSMEs)' na vituo rasmi vya huduma za kifedha kama vile tawi la benki, wakala, ATM n.k. Kulingana na utafiti wa Finscope 2023, kiwango cha watu wazima nchini Tanzania wanaozifikia huduma rasmi za fedha ndani ya kipenyo cha kilometa tano iliongezeka hadi asilimia 89 kutoka asilimia 86 mwaka 2017. Taarifa hizi pia upatikana katika Kanzidata ya Huduma za Fedha (FSR)

  2. Taarifa ya akaunti za akiba

    Taarifa ya akaunti za akiba zinaonyesha idadi ya akaunti za akiba za watu binafsi na biashara ndogo na za kati (MSMEs) katika taasisi rasmi za fedha. Tafiti zinaonyesha kuwa, utumiaji wa mawakala wa benki kumekuza sana tabia ya watu kujiwekea akiba na hivyo kusababisha kuongezeka kwa amana.

  3. Taarifa ya akaunti za huduma ya mikopo

    Taarifa ya akaunti za huduma za mikopo inaonyesha idadi ya akaunti za mikopo za watu binafsi na biashara ndogo na za kati (MSMEs) . Pia inajumuisha taarifa juu ya utumiaji wa mfumo wa marejeleo ya taarifa za mikopo. Taarifa hii ni muhimu katika kufikia kiwango cha upatikanaji wa mikopo kwa watu binafsi na biashara ndogo na za kati (MSMEs).

  4. Taarifa ya huduma za kujikinga na vihatarishi

    Taarifa ya huduma za kujikinga na vihatarishi inaangazia idadi ya akaunti za bima za watu binafsi na biashara ndogo na za kati (MSMEs). Taarifa hizi ni muhimu katika kusisitiza upatikanaji wa huduma kifedha na bidhaa ambazo huwezesha watu binafsi na biashara ndogo na za kati (MSMEs) kupunguza athari ya majanga na kujenga ujasiri katika biashara zao. Bofya ili Kufungua Taarifa na ripoti za kina za akaunti za bima zinapatikana katika tovuti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), https://www.tira.go.tz/

  5. Taarifa ya akaunti za huduma ya uwekezaji

    Taarifa ya akaunti za huduma ya uwekezaji inaonyesha idadi ya watu binafsi na biashara ndogo na za kati (MSMEs) wanaowekeza. Akaunti za huduma za uwekezaji zinaanzia kwenye akaunti za amana zinazotolewa na mabenki ili kuwekeza kwenye soko la mitaji na dhamana za serikali na za makampuni yaliyojisajili kwenye soko la mitaji na dhamana. Bofya ili Kufungua. Ripoti za kina za utendaji wa soko la dhamana zinapatikana katika tovuti ya Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana (CMSA) https://www.cmsa.go.tz/

  6. Taarifa ya huduma ya mifuko ya hifadhi ya jamii

    Taarifa ya huduma ya mifuko ya hifadhi ya jamii inaonyesha idadi ya watu walio na akaunti kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Taarifa hizi ni muhimu katika kuchanganua kiwango cha ufikiwaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii yenye huduma kama mafao ya kustaafu. Bofya ili Kufungua. Taarifa za kina za huduma ya mifuko ya hifadhi ya jamii zinapatikana katika tovuti yaa Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu na Wizara yenye dhamana ya Fedha (Zanzibar). https://www.kazi.go.tz/ & https://mofzanzibar.go.tz/newpofp/

  7. Taarifa ya huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi

    Taarifa ya huduma za fedha kwa njia ya simu za mkononi huonyesha idadi ya akaunti za watu binafsi wanaopata huduma za fedha kupitia simu za mkononi zinazotolewa na watoa huduma ya fedha kwa njia ya simu. Taarifa hizi ni muhimu katika kutathmini maendeleo ya upatikanaji na matumizi ya huduma za kifedha kidijitali nchini. Kwa taarifa ya kina za malipo kwa njia ya simu ya mkononi tembelea, https://www.bot.go.tz/PaymentSystem

  8. Takwimu za Mifuko ya Dhamana ya Mikopo

    Takwimu za Mifuko ya Dhamana ya Mikopo hutoa taarifa kuhusu Mifuko ya Udhamini wa Mikopo inayolenga kukuza na kusaidia sekta binafsi kwa kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa rasilimali fedha, ili kuchochea ajira na kuongeza mauzo nje ya nchim na hivyo kuchangia ukuaji wa uchumi.

  9. Taarifa ya utaratibu wa utatuzi wa malalamiko

    Takwimu ya utaratibu wa utatuzi wa malalamiko inatoa taarifa juu ya mifumo ya kushughulikia malalamiko ya watoa huduma za kifedha na utendaji kazi wake. Taarifa hizi ni muhimu kutathmini utendaji kazi wa kushughulikia malalamiko na huduma ili kuimarisha usalama wa watumiaji wa huduma za kifedha.