Skip to content
Jukwaa la Uthabiti wa Sekta ya Fedha Tanzania lakutana Dodoma

Jukwaa la Uthabiti wa Sekta ya Fedha Tanzania likiongozwa na Gavana Emmanuel Tutuba, limekutana leo katika makao makuu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dodoma. Jukwaa hilo limejadili masuala mbalimbali kuhusu sekta ya fedha nchini ambayo imeendelea kuwa thabiti kutokana na uwepo wa ukwasi wakutosha, kuimarika kwa shughuli za kiuchumi na kuboreshwa kwa hali ya biashara inayochochewa na sera madhubuti na hatua za udhibiti.

Jukwaa hilo linajumuisha mamlaka za uthibiti na wasimamizi wa sekta ya kifedha ikiwemo Wizara ya Fedha - Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Fedha na Mipango - Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tume ya Ushindani (FCC), Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania (TIRA) na Bodi ya Bima ya Amana(DIB).