Taarifa zinazotolewa kwenye tovuti hii zimechapishwa na Benki Kuu ya Tanzania kwa madhumuni ya kutoa taarifa na kuongeza uelewa kwa umma. Ingawa Benki hufanya juhudi zinazofaa kuhakikisha kuwa taarifa hizo ni sahihi na za wakati, haitoi dhamana, ya wazi au ya moja kwa moja, kuhusu usahihi, ukamilifu, uaminifu au uhalali wa taarifa hizo kwa madhumuni yoyote mahususi.
Taarifa zilizomo kwenye tovuti hii zinaweza kubadilishwa bila taarifa ya awali na hazipaswi kutegemewa pale ambapo taarifa rasmi za hivi karibuni zaidi zinapatikana kupitia sheria, kanuni, miongozo, waraka, matangazo au machapisho mengine rasmi ya Benki.
Benki Kuu ya Tanzania haitawajibika kwa hasara, madhara au athari yoyote itakayotokana na kutegemea taarifa zilizomo kwenye tovuti hii au zinazopatikana kupitia tovuti hii.
Tovuti hii inaweza kuwa na viunganishi vinavyoelekeza kwenye tovuti au vyanzo vya taarifa vya watu au taasisi nyingine. Viunganishi hivyo vimetolewa kwa urahisi wa watumiaji pekee na havimaanishi kuwa Benki Kuu imeidhinisha, imekubali au inapendekeza tovuti au vyanzo hivyo.
Benki Kuu ya Tanzania haiwajibiki kwa maudhui, usahihi, upatikanaji, usalama au taratibu za faragha za tovuti za watu au taasisi nyingine. Hakuna taarifa iliyo kwenye tovuti hii inayopaswa kutafsiriwa kuwa ushauri wa kifedha, kisheria, uwekezaji au ushauri mwingine wa kitaalamu, isipokuwa pale ambapo imeelezwa wazi hivyo.. watumiaji wanashauriwa kuthibitisha taarifa na Benki Kuu ya Tanzania au vyanzo vingine rasmi vinavyohusika kabla ya kuzitegemea.
Benki Kuu ya Tanzania ina haki ya kurekebisha, kusasisha, kusitisha au kuondoa maudhui au huduma yoyote inayopatikana kwenye tovuti hii wakati wowote na bila taarifa ya awali.