Taarifa kwa umma
Na. Jina la Waraka Tarehe ya Tangazo
1. MPANGO MKAKATI WA TAIFA WA HUDUMA JUMUISHI ZA FEDHA (2023-2028) 8/5/2023
2. COMMUNICATION FRAMEWORK (2023-2028) 8/5/2023
3. EVALUATION REPORT ON THE IMPLEMENTATION OF NFIF2 (2018-2022) 8/5/2023
4. GUIDE FOR FINANCIAL EDUCATORS (2023-2028) 8/5/2023
5. IMPLEMENTATION SUPPORT GUIDE (2023-2028) 8/5/2023
6. TAARIFA KWA UMMA: HATUA ZILIZOFIKIWA NA BENKI KUU YA TANZANIA KUHUSU FEDHA YA KIDIJITALI YA BENKI KUU 1/14/2023
Na. Nafasi Tarehe ya Tangazo


Watoa Huduma za Fedha wasiosajiliwa

Benki Kuu ya Tanzania imejizatiti katika kulinda ustawi wa kifedha na kuhakikisha wananchi wanafikiwa na watoa huduma za kifedha zilizo sajiliwa, simamiwa na kuaminika na Benki Kuu. Kutokana na jitihada endelevu za kuwalinda watumiaji wa huduma za kifedha, tuna leta Mfumo wa kutoa taarifa za watoa huduma wasioaminika au sajiliwa na Benki Kuu.

Watoa huduma za kifedha ambao hawajasajiliwa au ambao hawajaidhinishwa husababisha athari kubwa kwenye uthabiti na imani kwenye Sekta ya kifedha. Watoa huduma hawa wanaweza kushiriki katika shughuli za ulaghai ambazo zinaweza kuathiri ustawi wa kifedha wa watumiaji.

Benki Kuu inatambua wananchi kama wadau muhimu katika kuimarisha uthabiti na ufanisi wa sekta ya fedha. Kwa mantiki hii, utakapobaini mtu/taasisi yeyote anaetoa/inayotoa huduma za kifedha bila leseni halali au mwenendo unaotiliwa shaka katika sekta ya fedha, tafadhali toa taarifa kwa Benki Kuu mara moja. Utoaji wa taarifa hizi utasaidia kukulinda wewe na jamii kwa ujumla.

Ili kutoa taarifa za watoa huduma za kifedha ambao hawajasajiliwa, tafadhali tuma barua pepe kwa complaints-desk@bot.go.tz. Unaweza kutoa maelezo kama vile jina na eneo la taasisi, pamoja na taarifa yoyote muhimu ambayo inaweza kusaidia Benki katika kuchukua hatua zinazofaa.

Orodha ya watoa huduma wanaotiliwa shaka itahuishwa mara kwa mara kulingana na taarifa zinazo pokelewa kutoka kwa wananchi, baada ya kufanya tathmini ya kina. Orodha iliyohuishwa itapatikana kwenye tovuti ya Benki Kuu ili wananchi waweze kufanya rejea.

Usalama wa sekta ya fedha ni miongoni mwa vipaumbele muhimu vya Benki Kuu. Kwa kufanya kazi pamoja, tunaweza kuwezesha uwepo wa mazingira salama ya kifedha kwa kila mwananchi.

Wako katika ujenzi wa Taifa,

BENKI YA TANZANIA