Huduma jumuishi za kifedha huchangia katika ujumuishi wa kifedha katika sekta ya fedha, kwa mtu mmoja mmoja na biashara kufikiwa na kutumia bidhaa na huduma mbalimbali za kifedha zenye ubora wa hali ya juu kwa gharama nafuu ili kuboresha ustawi wa kifedha na kipato.
Huduma jumuishi za kifedha na ustawi huiwezesha Benki Kuu ya Tanzania kutimiza majukumu yake ya kusimamia utekelezaji wa sera ya fedha, kuboresha imani na uthabiti wa sekta ya fedha yenye hali nzuri ya kuwezesha maendeleo endelevu ya uchumi wa Taifa letu.
Benki Kuu kama Sekretarieti ya Baraza la Taifa la Huduma Jumuishi za Kifedha, inatekeleza na kuratibu mikakati ya huduma jumuishi za kifedha kama ilivyoainishwa kwenye Mpango Mkakati wa Huduma Jumuishi za Kifedha kupitia ushirikiano na ubia kati ya sekta ya umma na binafsi. Vilevile, Benki Kuu ina jukumu la kuwalinda walaji wa bidhaa na huduma za kifedha kwa taasisi zote inazozisimamia.