Mazingira ya Majaribio wa Ubunifu wa Teknolojia
Mazingira ya Majaribio ya Benki Kuu ya Teknolojia ya Fedha

Benki Kuu ya Tanzania (BOT) inakuza teknolojia ya fedha (FinTechs) na ubunifu kwa ajili ya kuongeza ufanisi katika kutoa huduma jumuishi za bidhaa na huduma za kifedha kwa kuweka mazingira wezeshi ya udhibiti. Mazingira ya Majaribio ya Teknolojia ya Fedha yanalenga kuweka mazingira maalum kwa ajili ya kufanya majaribio na kujifunza mbinu za kutoa bidhaa na huduma za kifedha ambazo bado hazijakidhi vigezo na kanuni zilizopo chini ya mamlaka ya Benki Kuu.

Waombaji wanaostahili kuwasilisha maombi ya kufanya majaribio ya bunifu za teknolojia ya fedha ni: watoa huduma za kifedha na makampuni ya teknolojia ya fedha.

Kwa maelezo zaidi juu ya vigezo na taratibu za maombi,

Tahadhari za Ubunifu wa Huduma Jumuishi za Kidigitali Zenye Kinga Dhidi ya Vihatarishi

Pia, Benki Kuu huchochkea ubunifu wa kifedha pamoja na kuwalinda watumiaji wa huduma za kifedha kwa kuwasiliana na umma kwa kutoa taarifa zinazohusiana na ubunifu wa teknolojia ya fedha. Mathalani, mwaka 2019, taarifa kwa umma ilitolewa ikiwatahadharisha juu ya kujihusisha na sarafu za kidigitali zisizotambuliwa na Benki Kuu. Januari 2023, taarifa kwa umma kuhusiana na hatua zilizofikiwa na Benki Kuu juu ya utoaji wa sarafu za kidigitali.


Kanzidata ya Taifa ya Huduma Jumuishi za Fedha

Benki kuu inatunza kanzi data ya Taifa ya huduma jumuishi za kifedha; inaendelea kufanya tafiti juu ya maeneo mapya ya ubunifu wa huduma jumuishi za fedha kwa njia ya kidigitali na kuendelea kuunda kanuni za kuchochea ukuaji wa ukuaji wa huduma za kifedha za kidigitali.


Kukuza Teknolojia ya Huduma Jumuishi za Kifedha

Watoa huduma za kifedha wanaongeza kasi ya matumizi ya teknolojia ya huduma za kifedha katika kusambaza bidhaa na huduma za kifedha ambazo zinafikika kwa urahisi, kwa gharama nafuu na zinazokidhi mahitaji ya wateja. Kwa kutambua majukumu ya Benki Kuu katika kufanikisha uthabiti wa sekta ya fedha na usalama kwenye mifumo ya malipo, Benki Kuu inakusudia kuhakikisha kwamba, ubunifu wa kiteknolojia katika sekta ya fedha unazingatia hatua za kukabiliana na hatari inayoweza kuvuruga hali ya uthabiti wa sekta ya fedha na kuzorotesha imani ya wateja kwenye huduma za kifedha.


Kanzidata ya Watoa Huduma za Kifedha

Kanzidata ya Watoa Huduma za Kifedha hutoa taarifa za mtawanyo wa kijeografia wa vituo vya kutolea huduma za kifedha nchini. Taarifa hizi husaidia katika kufanya tathmini ya ukaribu wa huduma za kifedha maeneo watu wanapoishi na kufanya miamala nchini. Vilevile, taarifa kuhusiana na mtawanyo wa kijeografia wa vituo vya kutolea huduma za fedha, huhabarisha watoa huduma za kifedha juu ya fursa za uwekezaji zilizopo https://fsr.bot.go.tz/home