Takwimu na Machapisho

Benki Kuu kwenye majukumu yake kama Sekretariati ya Baraza la Taifa la Huduma Jumuishi za Fedha ina wajibu wa kuratibu upatikanaji wa takwimu toka kwenye sekta ndogo ya kibenki, bima, masoko ya mitaji na dhamana, hifadhi ya jamii na huduma ndogo za fedha kwa mujibu wa mwongozo wa Mpango Mkakati wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha.


Data za Huduma Jumuishi za Kifedha

Data za huduma jumuishi za kifedha hukusanywa kwa kuzingatia vipimio vya maendeleo ya huduma jumuishi za kifedha vilivyomo kwenye Mpango Mkakati wa Huduma Jumuishi wa Kifedha. Data hizi hupatikana kwa wasimamizi wa sekta ya fedha na tafiti za watu na taasisi za wajasiriamali wadogo.


Machapisho

Benki Kuu ya Tanzania huchapisha ripoti za muda maalumu na ripoti nyinginezo kuhusu masuala yanayohusu upatikanaji na utumiaji wa bidhaa na huduma rasmi za kifedha.

Pia, kama Sekretarieti ya Baraza la Taifa la Huduma Jumuishi za Fedha, Benki Kuu ya Tanzania hutayarisha ripoti za huduma jumuishi za fedha kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Huduma Jumuishi za Fedha.

Na. Jina la Waraka Category Pakua
1. Mtaala wa Walimu Walioidhinishwa wa Fedha
Na. Jina la Waraka Category Pakua