Malengo na Majukumu
Malengo
  • Kuchochea sekta jumuishi ya fedha inayowezesha utekelezaji Madhubuti wa sera ya fedha, uthabiti na imani kenye sekta ya fedha
  • Kuimarisha imani na uhakika wa walaji katika matumizi ya bidhaa na huduma za fedha
  • Kuchochea ukuaji wa teknolojia ya fedha na ubunifu unaochochea huduma jumuishi za kifedha kwenye sekta ya fedha
  • Kukuza maendeleo ya sekta ya fedha kupitia ongezeko la ustawi katika upatikanaji wa mikopo na upanuzi wa huduma mbalimbali za kifedha

Majukumu
  • Kufanya kazi za Sekretarieti kwenye shughuli za huduma jumuishi za kifedha
  • Kuratibu wadau wa nchini, wa kikanda na wakimataifa kwenye masuala yanayohusiana na huduma jumuishi za kifedha na ustawi
  • Kuendesha shughuli za majaribio ya ubunifu wa teknolojia ya fedha
  • Kufanya tafiti kwenye masuala ya huduma jumuishi za kifedha
  • Kupokea na kutatua malalamiko ya walaji wa huduma za kifedha
  • Kufanya usimamizi wa mwenendo wa sekta ya fedha
  • Kutekeleza mikakati ya kutoa elimu ya fedha
  • Kusimamia utoaji wa dhamana kwa niaba ya Serikali