Mpango Mkakati, Kanuni, Nyaraka, Miongozo na Taratibu

Benki Kuu ya Tanzania, kama Sekretarieti ya Baraza la Taifa la Huduma Jumuishi za Fedha, imepewa jukumu la kuandaa na kutoa nyaraka zinazolenga, pamoja na mambo mengine, kutoa miongozo na kudhibiti mienendo mibaya kwenye sekta ya fedha. Katika kutekeleza jukumu hili, Benki Kuu, kwa kushirikiana na wadau wengine, huandaa mipango mkakati, kanuni, nyaraka, miongozo na taratibu juu ya masuala mbalimbali yanayohusiana na huduma jumuishi za kifedha, mfuko wa dhamana ya mikopo, na kumlinda mtumiaji wa huduma za kifedha.

Mipango mkakati ya Taifa hulenga kuratibu mikakati ya huduma jumuishi za kifedha kutoka kwa wadau mbalimbali zikiwemo wizara za kiserikali zinazohusiana na masuala ya huduma jumuishi za fedha, mamlaka za udhibiti, watoa huduma za kifedha, vyama vya kijamii na watoa huduma za kifedha pamoja na wadau wa maendeleo. Pia, ili kutoa mwongozo, kuimarisha nidhamu kwenye sekta fedha na kumlinda mtumiaji wa huduma za fedha, Benki Kuu hutoa kanuni, nyaraka, miongozo na taratibu;