Huduma Jumuishi za Kifedha
Hali ya Huduma Jumuishi za Kifedha Tanzania

Hivi karibuni, Tanzania imepitia mabadiliko makubwa kwenye sekta ya fedha ya kichochewa na kasi ya ongezeko la matumizi ya teknolojia katika kuzalisha na kusambaza bidhaa na huduma za kifedha. Mabadiliko haya, yanazidi kuifanya Tanzania kubaki kuwa mstari wa mbele ukanda huu kwenye masuala ya huduma jumuishi za kifedha. Pamoja na haya, bado upo uwiano usiosawia katika upatikanaji na matumizi ya huduma rasmi za kifedha nchi nzima kwa rika la watu wa wazima.

Ili kukabiliana na changamoto hizi, matumizi ya teknolojia ya kidigitali katika utuoaji wa huduma za fedha ili kuwa na wigo mpana wa kuyafikia makundi yasiyo na huduma, au yenye uhaba wa huduma rasmi za kifedha nchini. Katika kutekeleza majukumu haya, pamoja na mambo mengine, ilisaidia kupanua wigo wa upatikanaji na matumizi ya huduma rasmi za kifedha nchini. Kwa mujibu wa matokeo ya tafiti ya FinScope 2023, kiwango cha upatikanaji na matumizi ya huduma rasmi za kifedha kiliongezeka hadi kufikia 89% na 76% mwaka 2023 toka 86% na 65%, mtawalia. Hata hivyo, pamoja na mafaniko haya, kiwango cha watu walio nje ya huduma rasmi za kifedha bado kipo juu kwa baadhi ya makundi yakiwemo ya wakaazi wa vijijini, wakulima wadogo, vijana na wanawake.


Mikakati ya Huduma Jumuishi za Kifedha Tanzania

Katika kuendelea kutatua changamoto za huduma jumuishi za kifedha nchini, Baraza la Taifa la Huduma Jumuishi za Kifedha kupitia Sekretarieti huandaa Mpango Mkakati wa Huduma Jumuishi za Kifedha wa miaka mitano. Mpango Mkakati huu huanisha njia za kuyafikia malengo ya huduma jumuishi za kifedha kwa ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi. Mpango Mkakati wa Kwanza ulianza kutumika mwaka 2013 hadi 2017, huku Mpango Mkakati wa pili ukitumika kuanzia mwaka 2018 hadi 2022. Mpango Mkakati wa Tatu utaanza kutumika mwaka 2023 hadi 2028 (Kiungio).

Utekelezaji wa mipango mikakati hii husaidia katika kuyafikia malengo ya Taifa ya uchumi jumuishi kama yalivyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Dira ya Maendeleo ya Zanzibar 2050 na Mpango Mkuu wa Maendeleo ya Sekta ya Fedha wa miaka kumi (2020/21-2029/30).


Data za Huduma Jumuishi za Kifedha
Data za huduma jumuishi za kifedha hukusanywa kwa kuzingatia vipimio vya maendeleo ya huduma jumuishi za kifedha vilivyomo kwenye Mpango Mkakati wa Huduma Jumuishi wa Kifedha. Data hizi hupatikana kwa wasimamizi wa sekta ya fedha na tafiti za watu na taasisi za wajasiriamali wadogo.