Angalizo kwa watumiaji wa huduma za fedha
Orodha ya Kampuni na Tovuti
Orodha ya Tahadhari kwa Watumiaji wa Huduma za Kifedha (Orodha ya FCA) inatumika kama njia ya kuongeza uelewa kwa umma na kuhakiki watoa huduma za fedha waliosajiliwa ama kupewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania (bofya hapa) na hivyo kuwatofautisha na wale ambao wanadhaniwa kuwa wanaleseni leseni toka Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Orodha hiyo ya taasisi ambazo hudhaniwa kuwa zina leseni kutoka Benki Kuu inapatikana hapa (bofya hapa) ambayo huuishwa mara kwa mara kulingana na taarifa zinazotolewa na umma pamoja na tathmini ya kina inayofanywa kuhusu taasisi hizo. Wateja wanaweza kufuatilia orodha ya FCA kama mojawapo ya mbinu kadhaa za kubainisha kama taasisi au mtoa hudumua fulani wa fedha anatambuliwa ama ameidhi nishwa na BOT kutoa huduma za kifedha au huduma ambazo ziko chini ya udhibiti wa BOT.

Pia, Benki Kuu inahimiza umma kutembelea ukurasa wake wa wavuti wenye orodha ya watoa huduma wa kifedha waliopewa leseni na kusimamiwa na Benki Kuu ili kujihusisha na watoa huduma wa kifedha walio rasmi. Ili kupata orodha kamili ya taasisi za fedha za fedha zilizosajiliwa bofya hapa.

Benki Kuu ya Tanzania katika jukumu lake la kulinda watumiaji wa huduma za kifedha zilizo chini ya uangalizi wake, inaendelea kushirikiana na mamlaka nyingine kukuza imani na uaminifu katika sekta ya kifedha.