Kumlinda mtumiaji wa huduma za kifedha
Kumlinda mtumiaji wa huduma za kifedha

Benki Kuu imepewa jukumu la kulinda watumiaji wa huduma za kifedha. Wateja hulindwa ili kuongeza imani na uaminifu wao katika kutumia mifumo ya kifedha. Imani na uaminifu vinaweza kufikiwa kupitia uwazi wa taarifa, ulinzi wa taarifa za wateja, utoaji wa huduma kwa haki, utaratibu wa kusikiliza malalamiko kwa ufanisi na njia za kusuluhisha migogoro pamoja na utoaji wa elimu na uelewa wa masuala ya fedha.


Sheria za Benki Kuu ya Tanzania za kumlinda mteja wa huduma za kifedha, , 2019

Benki ilichapisha Sheria za Ulinzi wa Wateja wa Fedha, 2019 ili kuongoza watoa huduma za fedha kuweka utaratibu wa kushughulikia malalamiko kwa ufanisi ili kutatua malalamiko ya wateja. Aidha, sheria hizo zinakataza Watoa Huduma za Fedha kushiriki katika mienendo isiyo ya haki au yenye udanganyifu katika soko. Zaidi ya hayo, Benki inatekeleza ukaguzi wa tabia za soko nje ya ofisi na ndani ya ofisi ili kuhakikisha kuzingatia kwa sheria hizo.


Mbinu na zana za usimamizi wa miendeno ya soko

Mbinu na zana za usimamizi wa miendeno ya soko Madhumuni ya usimamizi wa masoko ni kuimarisha uwezo wa Benki Kuu katika kutambua na kupunguza hathari zinazoweza kusababishwa na mazoea mabaya ya soko yanayofanywa na Watoa Huduma za Fedha wasio waaminifu.


  • Ukaguzi wa ndani wa tabia za soko (onsite)
    Benki hufanya ukaguzi kwa kutembelea ofisi ya watoa huduma za kifedha ili kubaini uzingatiaji wa miongozo mbalimbali ya ulinzi wa wateja kama vile sekula, maelekezo maalum, viwango, na kanuni. Ukaguzi huu hufanyika kulingana na tathmini ya hatari ya taasisi husika kwenye mfumo wa fedha.
  • Ukaguzi wa nje wa tabia za soko (offsite)
    Benki hufanya ukaguzi wa nje kwa watoa huduma za kifedha kwa kufuatilia uzingatiaji wa miongozo mbalimbali ya ulinzi wa wateja kama vile sekula, maelekezo maalum, viwango, na kanuni. Ukaguzi huu hufanyika kulingana na tathmini ya hatari ya taasisi husika kwenye mfumo wa fedha.
  • Ukaguzi/ununuzi wa Siri (Mystery Shopping)
    Benki pia hufanya ununuzi wa siri ili kutambua matatizo katika soko, kuweka miongozo, na kufuatilia soko kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo. Hii hutekelezwa kwa hatua tofautitofauti kama vile kuelewa uzoefu wa wateja baada ya kuanzisha huduma au kanuni mpya, kuchunguza masuala maalum ya soko, au kufanya ukaguzi wa uzingatiaji wa sheria au kanuni zilizopo.

Mfumo wa Kushughulikia Malalamiko
Benki kuu ilianzisha dawati la kushughulikia malalamiko ya wateja wa huduma za kifedha kama njia ya gharama nafuu na yenye ufanisi ya kutatua malalamiko kati ya taasisi za kifedha na wateja wao. Benki hushughulikia malalamiko kutoka kwa taasisi za kifedha ili kuhakikisha ulinzi bora wa wateja nchini
  • Taratibu za kushughulikia malalamiko

    Kabla ya kuleta malalamiko Benki kuu, mteja atatakiwa kwanza kuwasilisha malalamiko ndani ya taasisi ya kifedha. Ili malalamiko yapokelewe, malalamiko hayo lazima yawe yamewasilishwa Benki Kuu ndani ya muda wa miaka miwili tangu kutokea kwa tukio la kusababisha malalamiko.

    Taasisi ya kifedha inapaswa kutatua malalamiko ya mteja ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kuleta malalamiko. Ikiwa haiwezi kutatua malalamiko ndani ya muda uliowekwa, itamjulisha mteja mara moja sababu za kushindwa kutatua ndani ya muda pamoja na hatua zinazochukuliwa kwa haraka kutatua malalamiko, na sio zaidi ya siku 7 baadaye.

    Endapo mteja akionekana kutokubaliana na uamuzi wa taasisi ya kifedha au akishindwa kupata jibu kutoka taasisi ya kifedha ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kuleta malalamiko, anaweza kuleta malalamiko yake Benki kuu ndani ya siku 14.

    Endapo mteja hatopendezwa na tabia za taasisi za kifedha, anaweza kuleta malalamiko yake kwa kufuata taratibu zilizotolewa katika kiunganishi, nyaraka au mfumo kwa lugha ya Kiingereza au Kiswahili.)

  • Taratibu za uamuzi

    Benki itatoauamuzi kuhusu suala hilo ndani ya siku 45 tangu tarehe ya kuleta malalamiko kwa Benki. Katika kutatua malalamiko, Benki inazingatia sheria husika, maamuzi ya kisheria, mkataba wa msingi, na miendeno ya sekta.

    Kama njia ya kurekebisha hali, Benki inaweza kumlazimisha taasisi ya kifedha kuomba msamaha, kubadilisha utaratibu/mazoea yake, kufanya malipo, au kulipa fidia kwa mlalamikaji kulingana na kesi husika.


Mipango ya Elimu ya Fedha na Ufahamu
  • Programu za mashuleni (On-schooling programs)
    Benki kama sekretarieti ya Baraza la Taifa la Kujumuisha Masuala ya Fedha kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia imeandaa nyezo za kusaidia kujumuisha elimu ya kifedha katika mfumo wa elimu nchini Tanzania (kutoka elimu ya msingi hadi vyuo vikuu).
  • Programu nje ya shule(Off schooling programs)
    Benki ya Tanzania kama sekretarieti ya Baraza la Taifa la Kujumuisha Masuala ya Fedha imeingia makubaliano ya ushirikiano na taasisi za kitaaluma zilizoteuliwa ili kutoa programu za kwa mafunzo kwa wakufunzi. Programu hii inalenga kutoa ithibati kwa waalimu/wakufunzi wa masuala ya fedha ambao hatimaye watasaidia katika kutoa elimu ya kifedha kwa umma.