Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, pamoja na Magavana 60 wa Benki Kuu kutoka mataifa mbalimbali duniani wamehudhuria Mkutano wa Mwaka wa 94 wa Taasisi ya Kimataifa ya fedha ya Benki Kuu uliofanyika Basel, Uswisi kuanzia tarehe 28 hadi 30 Juni 2024.
Gavana Tutuba pia alihudhuria mkutano wa Magavana wa Benki Kuu za Afrika ulioratibiwa na Kituo cha Utafiti wa Uchumi wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Oxford kuanzia tarehe 1 hadi 3 Julai 2024.
Mikutano hii hufanyika kila mwaka ambapo Magavana wa Benki Kuu hupata fursa ya kujadili masuala ya kifedha ya kimataifa na kikanda, kubadilishana uzoefu, na kushirikiana katika kutafuta suluhisho za changamoto mbalimbali za kiuchumi.