Dhamana za serikali za muda mfupi na za muda mrefu ni nyenzo zinazotumiwa na serikali kukopa fedha kutoka kwenye soko la fedha la ndani. Minada ya dhamana za serikali huendeshwa na Benki Kuu ya Tanzania kila wiki kwa niaba ya serikali kwa mfumo wa zabuni za ushindani na zisizo za ushindani. Minada hiyo hufanyika katika soko la awali na baadaye kuendelea kuuzwa au kununuliwa katika masoko ya upili. Dhamana za serikali huuzwa kwa njia ya minada na hufuata mfumo wa bei mbalimbali, yaani Wazabuni huruhusiwa kuleta zabuni nyingi kwa kila dhamana zinazoiva kwa kuomba kununua kwa bei tofauti. Minada inafanyika kulingana na kalenda ya mwaka ya mpango wa fedha wa serikali ambao hutangazwa na Benki Kuu ya Tanzania kila mwaka ili kuwawezesha wawekezaji kupanga mipango yao ya uwekezaji.
Kuna aina mbili ya dhamana za serikali yaani Dhamana za Muda Mfupi na Dahamana za Muda Mrefu au (Hati fungani). Dhamana za muda mfupi huiva ndani ya mwaka mmoja. Kwa kawaida huuzwa kwa bei chini ya shilingi 100 (Discount) na wakati wa kuiva mwekezaji hulipwa shilingi 100. Kiwango cha chini cha kuwekeza katika dhamana hizi ni shilingi 500,000 (Shilingi Laki Tano za Tanzania).
Dhamana za muda mfupi zinazotolewa na Benki Kuu ya Tanzania zinaiva katika vipindi vinne: siku 35, siku 91, siku 182 na siku 364.
Dhamana za muda mrefu (Hati fungani) hutolewa kwa ajili ya kugharamia hasa miradi ya maendeleo.. Hati fungani za serikali za muda mrefu zinazotolewa na Benki Kuu ya Tanzania kwa niaba ya serikali kwa sasa, zinaiva katika vipindi saba: miaka 2, miaka 5, miaka 7, miaka 10, miaka 15, miaka 20, na miaka 25. Zinatolewa katika kiwango cha riba isiyobadilika (Fixed rate/ Coupon)). Kiwango cha chini cha uwekezaji katika hati fungani za muda mrefu ni shilingi 1,000,000 (Shilingi milioni moja za Tanzania). Bei ya dhamana za muda mrefu zinaweza zikawa pungufu ya mia moja, sawa na mia moja na juu ya mia moja (Discount, Par Value and Premium prices). Kwa hivi sasa viwango vya gawio katika hati fungani za muda mrefu ni kama vifuatavyo:
Miaka
|
2 |
5 |
7 |
10 |
15 |
20 |
25 |
Gawio
|
7.60% |
8.60% |
9.48% |
10.25% |
11.15% |
12.10% |
12.56% |
Wakazi wote katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wana haki ya kushiriki katika minada ya dhamana za serikali.
Aina ya Wateja ni pamoja na:
- Taasisi
- Watu binafsi
- Watu wawili au zaidi (joint)
- Mtoto (Minor)
Kufungua Akaunti ya Dhamana za Serikali
Ili kushiriki katika minada ya Dhamana za Serikali, wawekezaji wote wanatakiwa wasajiliwe katika Mfumo wa Usajili wa Washiriki wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT-CDS). Usajili unafanywa kupitia Mawakala (CDPs). CDPs ni benki zote ambazo zina leseni ya kufanya biashara ya benki inayotolewa na Benki ya Tanzania na Mawakala (brokers/dealers) waliosajiliwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).
Mahitaji ya msingi ili Taasisi isajiliwe ni:
- Memorandum and Articles of Association (MERMATS),
- Cheti cha Usajili,
- Leseni ya Biashara,
- Picha za rangi za pasipoti za Wakurugenzi
- Katiba/Makubaliano/Uamuzi wa Kuanzisha
- Hati ya Msamaha wa Kodi (kama inahusika)
- Hati ya Namba ya Utambulisho ya Mlipakodi (TIN)
Mahitaji muhimu kwa ajili ya usajili wa watu binafsi na vikundi:
- Vielelezo vya utambulisho
- Picha mbili za rangi za pasipoti za hivi karibuni
- Hati ya Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN)
Key requirements for Minor registration are:
- Identification proof
- Birth certificate of Minor
- Two passport size photograph of minor and Two of guardian.
- Guardian shall sign across the photograph of the minor.
- Tax Identification Number (TIN) certificate of the Guardian
- In case the Guardian is not a natural parent to the minor, shall submit proof of guardianship
Benki Kuu ya Tanzania hutoa mwaliko kwa wawekezaji watarajiwa kuleta zabuni zao kwa mnada husika kwa njia ya Tangazo la Zabuni. Tangazo la Zabuni huchapishwa katika magazeti siku ya Ijumaa na kwenye tovuti ya Benki Kuu ya Tanzania ukurasa kwenye (CDS Web POrtal). MChakato wa zabuni unaanza mara tu baada ya Tangazo la Zabuni kuchapishwa na huendelea hadi saa 5.00 asubuhi siku ya mnada, ambayo kwa kawaida ni Jumatano.
Mteja atajaza fomu ya zabuni ya kuomba kushiriki katika mnada. Fomu iliyojazwa vizuri itawasilishwa kwa
Mawakala : wa Kushiriki katika Minada (CDPs). Mawakala watachukua maelezo yote na kuyaweka kwenye mfumo wa wawekezaji (CDS) na kuyawasilisha Benki Kuu ya Tanzania kwa njia ya mtandao.
Ili kuamua bei ya zabuni, wawekezaji wanatakiwa kuwa wafuatiliaji wa mwenendo wa bei za minada ya dhamana za serikali au kutumia huduma za washauri wa masuala ya kifedha au kupata mwongozo kutoka kwa mawakala wao.
Matokeo ya minada hutolewa kwa wastani saa moja baada kumalizika mchakato wa kununua zabuni siku ya mnada. Wawekezaji wanapata matokeo ya mnada kupitia kwa CDPs. Muhtasari wa Matokeo ya Mnada huonyesha taarifa muhimu zinazohitajika na wawekezaji katika kufanya maamuzi.
Note: Fedha zinahamishiwa tu BoT baada ya mwekezaji kutambua kwamba yeye ni miongoni mwa zabuni zilizofanikiwa katika mnada husika. Fedha za minada ya serikali hulipwa ndani ya siku moja baada ya mnada yaani T+1 (Yaani siku ya kazi inayofuata baada ya mnada).
Repurchase Agreements (REPO)
Katika kutekeleza sera ya fedha, Benki inatumia repo na reverse repo kama zana za kusimamia ukwasi. REPO), ni aina ya ukopeshaji wenye dhamana, wakati reverse REPO), ni aina ya dhamana ya kukopeshwais a form of collateralized borrowing.
Repurchase Agreements (REPO)Huu ni uuzaji wa dhamana za serikali kwa makubadiliano ya kurudisha dhamana hiyo baadaye kwa bei iliyokubalika. REPO hutumika kama njia ya kupunguza ukwasi wa ziada katika soko.
Reverse Repurchase Agreements (Reverse REPO) denotes the purchase of securities with a commitment to resell the securities at a future date and at an agreed price for purposes of injecting liquidity in the market.
Taarifa za Soko la Fedha za Kigeni kati ya Mabenki
Mnamo mwezi Juni 1994, Benki Kuu ilianzisha (IFEM) kama soko la jumla kuziwezesha benki za biashara na taasisi za fedha kufanya biashara ya fedha za kigeni miongoni mwao na hivyo kuamua kiwango rasmi cha kubadilisha fedha za kigeni kwa shilingi. IFEM ina mchango mkubwa katika kuamua kiwango rasmi cha kubadilisha fedha za kigeni na utekelezaji wa sera ya fedha. Benki Kuu hushiriki katika soko kama mnunuzi na muuzaji wa mwisho kabisa na huingilia katika soko ili tu kuleta utulivu katika kiwango cha kubadilisha fedha za kigeni. Idadi ya benki za biashara zinazoshiriki katika soko la jumla la fedha za kigeni ni 37, kati ya hizo benki 18 zinashiriki kupitia Reuters Dealing System. Mfumo wa bei ni wa pande mbili, yaani kila mshiriki anatakiwa aonyeshe bei yake (bid/ask quotes) (kwa kila dola za Kimarekani 100,000) ili kuongeza uwazi na kupunguza uoteaji katika soko.
Malengo ya msingi ya IFEM ni:
- Kuziwezesha benki za biashara na taasisi za fedha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya masoko na zana za fedha ili kuwahudumia wateja wao.;
- Kuongeza ufanisi katika mgawanyo wa akiba ya fedha za kigeni, ili kuwezesha upatikanaji wa viwango vya kubadilisha fedha za kigeni vinavyoamuriwa na soko;
- Kujenga mazingira bora ya uwekezaji kutoka nje, ambao mwishowe utapelekea kufunguliwa kwa soko la mitaji; na
- Kuimarisha utekelezaji wa sera ya fedha.