ORODHA YA MAJUKWAA AMBAYO HAYAJAIDHINISHWA NA BENKI KUU

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuchapisha orodha ya Majukwaa na Programu Tumizi zinazotoa huduma na mikopo ya kidijitali bila kuwa na idhini kutoka Benki Kuu. Chapisho hili linalenga kuutahadharisha na kuulinda umma dhidi ya hatari zinazohusiana na kujihusisha na wakopeshaji wa kidijitali ambao hawana leseni halali na vibali vya kutoa mikopo ya kidijitali.

Ifahamike kuwa kutoa mikopo ya kidijitali kuptia Majukwaa au Programu Tumizi za ukopeshaji wa kidijitali ambazo hazijaidhinishwa na Benki Kuu ni kosa la kisheria chini ya kifungu cha 16 cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya Mwaka 2018. Ikiwa itathibitika kuwa kuna mtu amejihusisha na Majukwaa na Programu Tumizi hizo zisizokuwa na kibali cha Benki Kuu, mtu huyo atakuwa katika hatari ya kukosa haki ya kinga ya ulinzi ya mtumiaji wa huduma za fedha kwa mujibu wa Kanuni za Benki Kuu ya Tanzania za Kumlinda Mtumiaji wa Huduma za Fedha za mwaka 2019 (kama zilivyorekebishwa).

Benki Kuu ya Tanzania inausihi umma kuziripoti mara moja Benki Kuu, Majukwaa na Programu Tumizi za utoaji wa mikopo ya kidijitali ambazo hazipo kwenye orodha ya taasisi za fedha zenye leseni au idhini ya utoaji wa mikopo ya kidijitali zilizochapishwa kwenye tovuti hii (List of Licensed Institutions), ili ziweze kuchukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa Sheria. Aidha, Benki Kuu itakuwa inahuisha orodha ya Majukwaa na Programu zisizokuwa na leseni au idhini ya kutoa mikopo ya kidijitali mara kwa mara pindi zitakapobainika na kuchukuliwa hatua za kisheria.

*** ORODHA YA MAJUKWAA NA PROGRAMU TUMIZI "APPLICATIONS" AMBAZO HAZIJAIDHINISHWA NA BENKI KUU KUTOA HUDUMA YA MIKOPO KIDIJITALI HADI KUFIKIA 31 DISEMBA 2025 ***