Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, ameshiriki katika ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF 2023).
Katika mkutano huo, mambo mbalimbali yanajadiliwa ikiwemo, ustawi wa sekta ya kilimo na mifumo ya chakula nchini. Mkutano huo, unafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 5 -8, Septemba, 2023.
Mkutano huo ulifunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango aliyezindua Ripoti ya Hali ya Kilimo Afrika. Pia, mkutano huo ulihusisha viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete, Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe na Waziri wa Uchumi wa Bluu Mhe. Suleiman Masoud.