Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, amekutana na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayesimamia masuala ya forodha, biashara na fedha, Bi. Annette Ssemuwemba na kujadili masuala mbalimbali kuhusu ustawi wa uchumi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki. Bi. Annette alifika kujitambulisha kwa mara ya kwanza tangu uteuzi wake Mei mwaka huu.
Hii ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Naibu Katibu Mkuu huyo, ambaye atatembelea Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi wanaoshughulikia masuala ya Forodha, Biashara, Fedha na Uwekezaji. aliyefika kujitambulisha kwa mara ya kwanza tangu uteuzi wake Mei mwaka huu.