BoT YATOA MAFUNZO KWA WADAU WA SEKTA YA FEDHA – ALAMA ZA USALAMA ZA NOTI ZETU

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inaendesha mafunzo ya utambuzi wa alama za usalama za noti zetu kwa wadau kutoka taasisi mbalimbali za fedha nchini ili kuwawezesha kudhibiti noti bandia.

Akizungumza katika mafunzo hayo yanayofanyika katika ofisi za tawi la BoT Arusha, kuanzia Agosti 28 mpaka Septemba 1, 2023, Meneja wa Idara ya Huduma za Sarafu BoT, Bw. Ilulu Ilulu, amezihimiza Benki za Biashara kuzingatia masharti  yaliyowekwa na Benki Kuu ya ubadilishaji wa noti chakavu .

Bw. Ilulu amezisisitiza Benki za Biashara kuzingatia kiwango cha asilimia 75 ya noti ambacho kimewekwa ili kuweza kuibadilisha noti chakavu au iliyochanika.

Aidha, washiriki wa mafunzo hayo wametakiwa kuelimisha umma kuhusu namna sahihi ya utunzaji wa noti/sarafu ili kuziwezesha kutumika kwa muda mrefu na kuipunguzia serikali gharama ya kuchapisha  noti/sarafu mpya ili kufidia zilizoharibika