Balozi wa Oman nchini Tanzania, Mhe. Saud Al Shidhani, amekutana na Gavana wa Benki Kuu Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, katika Ofisi za Makao Makuu Ndogo Dar es Salaam, ambapo wamezungumza masuala mbalimbali kuhusu Ustawi wa Sekta ya Fedha kupitia mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Oman.
Kwa upande wake Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, amesisitiza, BoT kama taasisi inayosimamia Sekta ya Fedha, itatoa ushirikiano kwa sekta ya fedha ya Oman kwa lengo la kuchagiza ustawi Sekta hiyo ikiwemo sekta ya mabenki, kwa nchi zote mbili.