Muhtasari kuhusu mifumo ya Malipo

Kila siku watu, biashara na serikali wanabadilishana huduma au bidhaa ili kupata fedha. Kwa hio Fedha inatumika kama njia ya kubadilishana. Hivyo, Mfumo wa malipo ni njia inayotumika kuhamisha fedha toka kwa muuzaji kwenda kwa mnunuzi.

Nchini Tanzania, fedha taslimu ndio njia maarufu ya kufanya malipo. Hata hivyo kuna njia nyingine mbalimbali za kufanya malipo kama vile hundi promisory notes, bills of exchange, malipo ya kielektroniki, malipo ya kadi, malipo kwa njia ya mtandao na malipo kwa njia ya simu.

Benki Kuu ya Tanzania imekasimiwa mamlaka na Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa yam waka 2015 na Sheria ya Benki Kuu yam waka 2006 kusimamia na kudhibiti mifumo na huduma za malipo kwa watoa huduma za fedha yakiwemo mabenki na taasisi nyingine za fedha.

Benki Kuu ya Tanzania inashirikiana na wadau mbalimbali katika kuboresha usalama na uendeshaji mzuri wa mifumo ya malipo nchini. Wadau hawa wanajumuisha Taasisi za kifedha, watoaji wa huduma za miundombinu ya malipo kama vile kampuni za simu, watumiaji wa huduma za malipo kama vile watu binafsi, makampuni, serikali, mamlaka za udhibiti katika sekta za fedha kama Soko la hisa la Dar es Salaam, watoaji wa huduma za mifumo ya malipo kama SWIFT, watoaji wa huduma za malipo kwa njia ya kadi, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana Mamlaka za Kifedha Kikanda na Kimataifa kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki, Shirika la Fedha la Dunia na Benki ya Dunia.