Sheria na Kanuni

Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa ya mwaka 2015 inatoa mamlaka kwa Benki Kuu ya Tanzania kusimamia na kudhibiti mifumo ya malipo na kuboresha mifumo ya kibenki na taasisi za kifedha iwe ya kuaminika, ili kuwezesha malipo kufanyika kwa maendeleo ya uchumi wa taifa. Sheria hiyo inaongezewa nguvu na Sheria ya Benki Kuu ya mwaka 2006 ambayo inatoa mamlaka mapana kwa Benki Kuu kusimamia bidhaa na huduma za mifumo ya malipo zinazotolewa na mabenki na taasisi zingine.

Benki Kuu ya Tanzania inatoa waraka na miongozo ili kuhakikisha kwamba shughuli za mifumo ya malipo inafanyika vizuri. Wadau mbalimbali wanashirikishwa pia katika utengenezaji wa sheria na kanuni za mifumo ya malipo.