Mifumo ya Malipo.

Benki Kuu ya Tanzania ina jukumu la kuwa wakala wa kuwezesha malipo kufanyika baina ya watoa huduma za malipo kama vile benki na watoaji wa huduma za malipo kwa njia ya kadi. Hii inamaanisha ulipanaji na badilishanaji wa fedha au thamani yoyote kwa ajili ya amana. Hii pia inajumuisha kusahishisha akaunti za watoa huduma za malipo waliofanya biashara na kuweka namna ya kuhamisha fedha na amana. Benki Kuu ya Tanzania inawezesha malipo ndani ya nchi ambayo ni makubwa au ya haraka kupitia mfumo ujulikanao kwa jina la Tanzania Interbank Settlement System (TISS). Vilevile Benki Kuu ianwezesha malipo ya hundi au malipo madogo ya kielektroniki kupitia mfumo wa malipo uitwao Tanzania Automated Clearing House (TACH).

Benki Kuu inawezesha pia malipo nje ya nchi kwa nchi wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki (EAC) kupitia mfumo wa malipo uitwao East Africa Payment System (EAPS). Vilevile Benki Kuu inasimamia mfumo wa malipo nje ya nchi baina ya nchi wanachama wa Jumuia ya maendeleo Kusini mwa Afrika ujulikanao kama SADC RTGS.