Malengo ya Mifumo ya Malipo ya Taifa
  • Kuhakikisha kuwa kuna mifumo ya malipo ya taifa ya kuaminika, salama, rahisi, yenye gharama nafuu na iliyounganishwa ili kukidhi mahitaji ya kiuchumi.
  • Kuboresha uwezo wa nchi kusimamia uchumi mdogo mdogo kwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati juu ya hisa na mzunguko wa fedha.
  • Kuwezesha ubadilishanaji na makubaliano ya kifedha na dhamana ili kupunguza fedha iliyo kwenye mzunguko na kuboresha ufanisi katika mzunguko na upelekaji wa fedha.
  • Kutanua wigo katika mifumo ya malipo kwa kuzingatia maendeleo ya teknolojia kutegemeana na mahitaji ya watumiaji.
  • Kuhakikisha uwepo wa mifumo ya kisheria na kitaasisi iliyo imara na yenye ufanisi inayoweza kusimamia mifumo ya malipo.
Kazi ya Benki Kuu katika Mifumo ya Malipo ya Taifa
  • Kutengeneza sera za mifumo ya malipo ya Taifa kulingana na mahitaji mbalimbali ya sekta zote nchini.
  • Kutambua majukumu ya msingi ya mifumo ya malipo ambayo wadau mbalimbali, ikiwamo Benki Kuu ya Tanzania, wanatakiwa kuyafanya katika kuendeleza, kutekeleza, kuendesha, na kusimamia mifumo ya malipo ya Tanzania.
  • Kuishauri Serikali na jamii juu ya Mambo yanayohusu mifumo mbalimbali ya Malipo.
  • Kuratibu, kuoanisha na kuridhia mchakato wa viwango na mikakati ya pamoja ya mifumo ya malipo katika ngazi ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa.
  • Kuiwakilisha nchi katika majukwaa ya Kitaifa na Kimataifa kuhusu Mifumo ya Malipo.
  • Kuwasiliana moja kwa moja au kupitia Kamati za Mifumo ya Malipo ya Taifa na wadau na vyombo vya kimataifa kama vile BIS, Benki ya Dunia, SADC, EAC, na washauri wengine.
  • Kuhakikisha kwamba Mifumo ya Malipo iliyopo ikiwamo Miundo na Sheria inasimamiwa, kudumishwa na kuzingatiwa ipasavyo.
  • Kutoa leseni na vibali vya kutoa huduma za mifumo ya malipo kulingana na Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa
  • Kuhakiki na kushauri juu ya huduma mpya za mifumo ya malipo na vile vile kutengeneza miongozo juu ya matumizi na uanzishwaji wa huduma hizo.
  • Kuandaa kampeni na vipindi mbalimbali vya uhamasishaji, kuhusu mifumo yote mipya ya malipo