Payment Systems Initiatives.

Muingiliano wa Huduma Jumuishi za Kifedha

Sekta ya mifumo ya malipo nchini Tanzania linakua na hivyo kuwepo umuhimu wa wadau kufany kazi pamoja. Kuna manufaa kadhaa yanayoletwa na muingiliano wa huduma za kifedha ikiwemo urahisi wa malipo, uharaka, gharama ndogo na usalama wa kufanya malipo. Benki Kuu ya Tanzania kama msimamizi wa mifumo ya malipo ni mdau katika jambo hili. Benki Kuu inatoa ushauri na kuunda sera katika kuhakikisha usalama wa malipo kwa wadau husika. Mpaka sasa watoaji huduma za malipo wanatumia makubaliano kati ya mtoa huduma mmoja na mwingine katika kufanya malipo baina ya wateja wao.

Benki Kuu ya Tanzania kwa hivi sasa inatekeleza mradi wa kutengengeza mfumo jumuishi wa haraka wa kufanya malipo kati watoa huduma wa mifumo ya malipo ujulikanao kama Tanzania Instant Payment System (TIPS) ambao unatarajiwa kuanza kufanya kazi mwezi Juni 20120. TIPS ni mfumo jumuishi wa kieletroniki utakaoendesha na Benki Kuu ya Tanzania utakaowezesha kuhamisha fedha baina ya watoa huduma tofauti kama vile benki na kampuni za simu. TIPS itawezesha malipo ya papo kwa hapo kati ya watoa huduma za kifedha. TIPS itaongeza huduma jumuishi ya kifedha kwa kuboresha upatikanaji na matumizi ya huduma za kifedha nchini kutokana na kuwezesha muingiliano wa huduma kati ya watoa huduma za kifedha. TIPS itawezesha mfumo thabiti wa kufanya malipo kati ya watoa huduma za kifedha kwa njia ya kielekytroniki. TIPS itaongeza ubora kwa kuondoa njia ya sasa ya makubaliano kati ya watoa huduma na kueka mfumo wa pamoja kwa watoa huduma wote kufanya malipo.

Maboresho ya Mfumo wa Malipo wa TISS

Kutokana na mabadiliko katika teknolojia na masoko ya fedha, ulazima wa kuwa na mifumo salama ya malipo ni kipaumbele kwa benki kuu nyingi duniani. Benki Kuu ya Tanzania ipo katika juhudi endelevu za kuiboresha Mifumo yake ya malipo ili kuhakikisha usalama, uhakika na uharaka wa malipo. Mradi wa maboresho ya mfumo wa sasa wa TISS utawezesha kuhimili mabadiliko katika soko.

Kuanzisha daftari la vituo vya kutoa Huduma za Kifedha

Benki Kuu ya Tanzania inatekeleza mradi wa kutengeneza dafatri kuandikisha vituo vya Huduma za Kifedha (FSR) ambalo litawianisha mahali na aina ya huduma za kifedha zinatolewa. Rejista hii itatumia teknolojia ya GPS katika kuonyesha sehemu zote za umma ambapo huduma za kifedha zinatolewa na aina ya huduma inayotolewa. FSR imetengenezwa kuwasaidia wadhibiti kutengeneza sera na pia kufuatilia malengo ya kitaifa juu ya huduma jumuishi za kifedha. FSR pia itawasaidia watoaji wa huduma za kifedha kutambua maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma mbalimbali za kifedha.

FSR itatoa taarifa hizi za vituo vya huduma za kifedha kwa wadau mbalimbali kulingana na mahitaji ya makundi kama vile Umma, Watoaji wa huduma za kifedha, na Wadhibiti kupitia tovuti.

Huduma na sehemu zifuatazo zitahifadhiwa katika FSR

 • Matawi ya benki
 • Wakala wa benki
 • ATMs
 • Wakala wa Pesa
 • Taasisi ndogo za kifedha
 • Wafanyabiashara wa huduma za kibenki
 • Wafanyabiashara wa huduma za Pesa
 • Watoaji wa huduma za Bima
 • SACCOS
 • Watoaji wa kati wa huduma za malipo
 • Maduka ya kubadilisha fedha
 • Masoko ya Mitaji na Amana
 • Huduma za bima ya afya