Nyenzo na Utekelezaji wa Sera ya Fedha

Benki Kuu inatelekeleza mfumo wa sera ya fedha  unaolenga kiasi cha pesa  katika uchumi. Katika mfumo huu Benki Kuu hulenga kiasi cha pesa taslimu na hivyo kuamua kiasi cha ujazi wa fedha katika uchumi  ili kufikia malengo husika ya sera ya fedha.

  • Lengo la Utekelezaji
  • Malengo ya Kati

Lengo la Utekelezaji

Ujazi wa fedha hutumika kama lengo la kati kwa kuwa ukuaji wake una mahusiano ya karibu na lengo la msingi la sera ya fedha la kuhakikisha utulivu wa bei. Sera ya fedha inayotekelezwa na Benki Kuu ya Tanzania ina lengo kuu la kuhakikisha uwepo wa utulivu wa kasi ya mfumuko wa bei nchini. Sera ya fedha hutekelezwa kwa kudhibiti kiwango cha ukuaji wa fedha taslimu (lengo la uendeshaji), na hatimaye ukuaji wa ujazi wa fedha (lengo la kati) ili kufikia lengo la msingi la sera ya fedha.

Malengo ya Kati

Ujazi wa fedha hutumika kama lengo la kati kwa kuwa ukuaji wake una mahusiano ya karibu na lengo la msingi la sera ya fedha la kuhakikisha utulivu wa bei. Sera ya fedha inayotekelezwa na Benki Kuu ya Tanzania ina lengo kuu la kuhakikisha uwepo wa utulivu wa kasi ya mfumuko wa bei nchini. Sera ya fedha hutekelezwa kwa kudhibiti kiwango cha ukuaji wa fedha taslimu (lengo la uendeshaji), na hatimaye ukuaji wa ujazi wa fedha (lengo la kati) ili kufikia lengo la msingi la sera ya fedha.

Ili kutimiza lengo hilo Benki Kuu hutumia nyenzo mbalimbali hususan uuzaji wa dhamana za serikali,mikataba ya kukopesha fedha baina ya Benki Kuu na benki za biashara, uuzaji na ununuzi wa fedha za kigeni, na kikawango cha chini cha kisheria cha hifadhi ya amana za benki za biashara Benki Kuu. Mbali na nyenzo za sera ya fedha, Benki Kuu kupitia njia mbalimbali kama vile dirisha la Lombadi, na Discount, na kutoa nafasi kwa benki za biashara kupata mikopo maalum na ukwasi ili kukidhi mahitaji yao kwa vipindi vifupi vifupi visivyozidi siku 90.

Benki Kuu ya Tanzania hutumia nyenzo mbalimbali za sera ya fedha kupitia nguvu ya soko huria. Nyenzo hizi za sera ya fedha zinazotegemea nguvu ya soko zimekuwa zikitumika tangu kuasisiwa kwa mfumo huria wa usimamizi wa uchumi katikati ya miaka ya 1990. Nyenzo za sera ya fedha zinazotumiwa na Benki Kuu ya Tanzania ni pamoja na uuzaji wa dhamana za serikali,mikataba ya kukopesha fedha baina ya Benki Kuu na benki za biashara, uuzaji na ununuzi wa fedha za kigeni, na kikawango cha chini cha kisheria cha hifadhi ya amana za benki za biashara Benki Kuu. Mbali na nyenzo za sera ya fedha, Benki Kuu kupitia njia mbalimbali kama vile dirisha la Lombadi, na Discount, na kutoa nafasi kwa benki za biashara kupata mikopo maalum na ukwasi ili kukidhi mahitaji yao kwa vipindi vifupi vifupi visivyozidi siku 90.

Uendeshaji wa Soko Huru/la Wazi

Katika uendeshaji wa soko la wazi, benki kuu nyingi hutumia njia kuu mbili zenye malengo tofauti. Njia ya kwanza hutumika pale benki kuu inapokuwa na lengo la kufikia kiwango fulani cha fedha taslimu, na wakati huo huo kuruhusu kiwango cha riba kubadilika badilika kwa uhuru. Njia hii hasa hutumika katika uendeshaji wa soko la upili ambalo halina ufanisi na soko la fedha baina ya benki za biashara. Njia hii inatoa nafasi kwa benki kuu kufafanua lengo lake kwa uwazi zaidi, hasa pale ambapo inakuwa na lengo kuu la kudhibiti wa mfumuko wa bei. Njia ya pili hutumika pale ambapo benki kuu inalenga kiwango maalum cha riba, na wakati huo huo kuruhusu kiwango cha pesa taslimu kubadilika badilika kwa uhuru. Kwa kulinganisha na njia ya kwanza, njia hii ya pili hutumika zaidi pale ambapo kuna masoko bora ya fedha yenye ufanisi wa hali ya juu, pamoja na utumiaji mkubwa wa teknolojia kwenye shughuli za uendeshaji wa masoko ya fedha. Benki Kuu ya Tanzania hutumia uendeshaji wa soko la wazi kama nyenzo kuu katika utekelezaji wa sera ya fedha kwa kuuza dhamana za serikali.

Soko la Fedha za Kigeni

Uendeshaji wa soko la fedha za kigeni unafanywa kwa ushirikiano baina ya Benki Kuu na benki za biashara. Katika soko hili Benki Kuu hununua na kuuza fedha za kigeni kwa benki za biashara. Soko hili ndio msingi wa upatikanaji wa kiwango cha ubadilishaji wa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya fedha za kigeni. Bila kuathiri lengo kuu la utulivu wa bei, Benki Kuu huchukua hatua za makusudi za aidha kununua fedha za kigeni kwa lengo la kuimarisha akiba ya taifa ya fedha za kigeni, au kuuza fedha za kigeni hatua ambazo zinasaidia kupunguza kasi kubwa ya kubadilika badilika kwa viwango vya ubadilishanaji wa shilingi na fedha za kigeni kwenye uchumi.

Hitaji la Kisheria kwa Mabenki kuhusu Hifadhi ya Sehemu ya Amana

Ili kusimamia uwezo wa benki za bishara katika kuongeza ukwasi kwenye uchumi, benki hizi zinatakiwa kisheria kuhifadhi sehemu ya amana za wateja wake kwenye akaunti maalum zinazofunguliwa Benki Kuu kwa lengo la kuhakikisha utulivu wa bei. Kwa kawaida, benki kuu hutumia akiba hizo za mabenki kama moja ya nyenzo za kuhakikisha utulivu wa bei.

Riba ya Mikopo ya Benki Kuu

Kiwango cha riba ya mikopo (discount rate) hutumika na Benki Kuu kwa mikopo inayotolewa kwa serikali na mabenki. Benki Kuu huweka kiwango cha juu cha riba kwa mikopo yake kwa mabenki na serikali inapokuwa inatekeleza sera ya fedha ya kubana ukwasi (tight monetary policy). Kwa kuwa Benki Kuu ya Tanzania hutumia uendeshaji wa shughuli za soko la wazi (OMO) kama njia kuu ya utekelezaji wa sera ya fedha, kiwango chake cha riba kiko juu sana ili kuwakatisha tamaa wakopaji kutumia njia hiyo kupata fedha. Hivi sasa, kiwango hicho kiko juu kwa asilimia 5 ya wastani wa riba inayotolewa kwa hati fungani zote za muda mfupi zinapoiva.

Ushawishi

Benki Kuu hutumia njia ya mazungumzo na mijadala kwa lengo la kushawishi wadau katika masoko ya fedha, hasa benki za biashara, katika kupanga viwango vya riba za amana na mikopo. Nyenzo hii hutumiwa kwa pamoja na nyenzo zingine za sera ya fedha.

Makubaliano ya Hiari

Haya ni makubaliano ya hiari kati Benki Kuu ya Tanzania na benki za biashara yanayolenga kuimarisha hali ya fedha katika uchumi. Makubaliano kama hayo yanafikiwa kati ya Benki Kuu na benki kubwa za biashara katika jitihada za kupunguza tofauti ya viwango vya riba za mikopo na amana.