Dhima, Dira na Tunu za Shirika

Dhima yetu
“ Kudumisha utulivu wa bei na uadilifu katika sekta ya fedha kwa ukuaji wa jumuishi wa uchumi ”

Dira yetu
“ Kuwa msimamizi anayehakikisha utulivu wa uchumi na mfumo wa kisasa wa kifedhaili kuendelea kuimarisha nchi katika ngazi ya uchumi wa kati na zaidi .”


Tunu za Shirika
Tunu za Benki zinaonesha namna tunavyotekeleza majukumu yetu na kushirikiana na wadau wetu. Kwa hiyo,kwa wakati wote tunaongozwa na tunu zifuatazo:

Uadilifu:
Tunatekeleza majukumu yetu kwa uadilifu unaojionesha katika uaminifu, utii, ukweli na usiri.

Utendaji wa Mfano:
Tunatimiza wajibu wetu kwa umahiri na ubunifu ili kuboresha ufanisi wa shirika.

Uwajibikaji
Tunawajibika binafsi na kwa pamoja katika kutekeleza majukumu yetu.

Uwazi:
Tunatekeleza majukumu yetu kwa usahihi, uwazi na kuwasilisha taarifa muhimu kwa wadau wetu.

Ushirikishwaji:
Tunathamini ushirikishwaji mpana, utendaji kazi wa pamoja na kubadilishana ujuzi na uzoefu katika kutekeleza majukumu yetu.