Muundo wa Taasisi

MUUNDO WA BENKI KUU YA TANZANIA

Muundo wa taasisi hii umegawanyika katika sehemu nne kama unavyoonekana hapa chini:

a. Bodi ya Wakurugenzi

Bodi ya Wakurugenzi ndiyo chombo cha juu kabisa cha maamuzi Benki Kuu (BoT). Bodi inapata mamlaka yake kutoka katika Sheria iliyoanzisha Benki Kuu ya Tanzania. Katika nafasi hiyo, Bodi ina mamlaka ya mwisho kwa utendaji Benki Kuu.

Bodi ya Wakurugenzi ni chombo chenye madaraka na mamlaka ya juu kabisa kinachotoa maamuzi ya kisera katika muundo wa Benki Kuu ya Tanzania. Inapata mamlaka kutoka katika Sheria iliyoanzisha Benki Kuu.

Muundo wa Bodi ya Benki Kuu ni kama ifuatavyo:

  • Gavana (Mwenyekiti)
  • Manaibu Gavana watatu, Makamu Mwenyekiti, kwa mfuatano atakaoamua na Gavana wa Benki
  • Mwakilishi wa Wizara ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
  • Wakurugenzi wanne wasio watendaji; na
  • Katibu wa Bodi.

b. Ofisi Kuu:

Ofisi Kuu ya BoT inamhusu Gavana akisaidiwa na Manaibu Gavana watatu; Naibu Gavana (Utawala na Udhibiti wa Ndani), Naibu Gavana (Sera za Uchumi na Fedha) na Naibu Gavana (Usimamizi na Uthabiti wa Sekta ya Fedha).

Viongozi wote wa Ofisi Kuu wanasimamia Kurugenzi mbalimbali kama ifuatavyo:

Ofisi ya Gavana - Kurugenzi ya Huduma za Sheria, Kurugenzi ya Ukaguzi wa Ndani, Idara ya Mawasiliano, Idara ya Usimamizi wa Ununuzi na Kitengo cha Huduma za Uchunguzi

Ofisi ya Naibu Gavana (Utawala na Udhibiti wa Ndani) – Kurugenzi ya Fedha, Kurugenzi ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Kurugenzi ya Usimamizi wa Majengo na Vifaa, Kurugenzi ya Mifumo ya Mawasiliano,  Idara ya Usimamizi wa Vihatarishi, Idara ya Mipango, Idara ya Usalama wa Ndani na Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania.

Ofisi ya Naibu Gavana (Uchumi na Sera) - Kurugenzi ya Utafiti na Sera za Uchumi, Kurugenzi ya Masoko ya Fedha, Kurugenzi ya Usimamizi wa Sarafu, Kurugenzi ya Huduma za Kibenki, Matawi ya Benki Kuu.

Ofisi ya Naibu Gavana (Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha) - Kurugenzi ya Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, Kurugenzi ya Uthabiti na Ujumuishi wa Fedha na Idara ya Uthabiti wa Fedha

c. Menejimenti

Hii inaundwa na Wakurugenzi, Mameneja na mameneja wasaidizi ambao wanaongoza Kurugenzi, Idara na Vitengo mbalimbali.

d. Wafanyakazi

Benki Kuu ina wafanyakazi katika makundi manne: Wataalamu Daraja la kwanza, Wataalamu Daraja la Pili, Makarani na Wasaidizi wanaowezesha utekelezaji wa majukumu ya Benki Kuu kikamilifu.