Noti na Sarafu Zilizochakaa

Fedha zilizoharibika ni fedha ambazo zimechakaa na haziwezi tena kutumika katika mzunguko. Fedha hizi hupoteza mwonekano, ni ngumu kutambua uhalali wake na mara nyingi huharibika kutokana na sababu mbalimbali kama maji, moto, madawa n.k. Fedha hizi mbovu zikiwasilishwa Benki Kuu, Idara ya sarafu huzipokea na kuzibadilisha na fedha mpya kwa thamani ile ile. Fedha chakavu inayopokelewa na kubadilishwa na Benki Kuu inatakiwa kuwa na sifa zifuatazo:

  • Isiwe imeharibiwa makusudi
  • Iwe ni pesa halali
  • Iwe na ukubwa wa asilimia 75% au zaidi
  • Iwe na angalau namba za upande mmoja