Huduma za Kibenki

Benki Kuu ya Tanzania ni benki inayohudumia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar. Pia ni benki ya taasisi za umma na benki za biashara. Kazi hizi ni kwa mujibu wa Sheria ya Benki Kuu ya Tanzania ya mwaka 2006. Hivyo, kama benki na wakala wa huduma za kibenki, Benki Kuu inatoa huduma zifuatazo:

  1. Kupokea na kutunza amana za Serikali na taasisi za umma;
  2. Kusimamia na kuziendesha akaunti za Serikali, kufanya malipo, kuhamisha pesa kutoka katika akaunti hizo na kukusanya mapato ya Serikali;
  3. Kutunza na kuendesha akaunti maalum kwa mujibu wa makubaliano baina ya Benki Kuu na Serikali au taasisi za umma husika;
  4. Uwakala wa Serikali katika kulipa madeni ya umma, pamoja na kulipa riba kwenye dhamana za serikali na dhamana zingine za Serikali;
  5. Kulipa, kutoa, kukusanya au kupokea amana au mifuko nchini Tanzania au nje;
  6. Nunua, uza, hamisha au pokea hundi, bills of exchange na dhamana zingine;
  7. kusanya mapato, ya msingi au riba, kutokana na mauzo yanayotokana na hisa za setikali au taasisi za umma (accruing to the interest of), au mali nyingine; na
  8. Nunua, uza,hamisha au pokea kwa ajili ya kutunza dhahabu au fedha za kigeni

Pia, Benki inatoa huduma kwa benki za biashara kwa:

  1. Kufungua akaunti, kupokea malipo mbalimbali na pesa kutoka kwenye mabenki hayo ajili ya utunzaji;
  2. ii. Inatoa huduma ya kuziwezesha benki kubadilishana zana za malipo (interbank services);
  3. Kutoa huduma ya kuhifadhi
  4. Kutoa mikopo ya muda mfupi (Lombard) kwa mabenki

Ili kuboresha utoaji wa huduma za kibenki, Benki Kuu imekuwa ikiboresha miradi kuelekea utoaji wa huduma muhimu kidigitali. Lengo kuu ni kuongeza ufanisi na kukidhi mahitaji ya wateja.