Financial Sector Supervision
Utangulizi
Benki Kuu ya Tanzania ina mamlaka ya kutoa leseni, kudhibiti na kusimamia benki na taasisi za fedha zikiwemo benki za biashara, taasisi za huduma ndogo za fedha, benki za jamii, benki za maendeleo, kampuni za karadha, taasisi za mikopo ya nyumba, watoa huduma ndogo za fedha, taasisi za taarifa za wakopaji, maduka ya kubadilisha fedha za kigeni na ofisi za uwakilishi za benki zilizoko nje. Pia, Benki Kuu ina wajibu wa udhibiti na usimamizi wa masuala ya kifedha (uwekezaji) wa mifuko ya hifadhi ya jamii nchini Tanzania. Jukumu la msingi katika udhibiti na usimamizi wa taasisi za fedha ni kuhakikisha kuna uthabiti, usalama na ufanisi wa mfumo wa fedha na kupunguza uwezekano wa wenye amana kupata hasara.