Sheria na Kanuni

Benki Kuu ya Tanzania inadhibiti na kusimamia benki, taasisi za fedha, taasisi za mikopo ya nyumba, kampuni za karadha, taasisi za taarifa za wakopaji na Maduka ya Kubadilisha Fedha za Kigeni. Benki Kuu inaanda miongozo kwa taasisi za fedha ambayo inatekelezwa  kupitia Kanuni, Miongozo na Nyaraka (Maelekezo na Notisi). Miongozo imetayarisha pia ili kuhamamisha uendeshaji mzuri katika taasisi hizo. Pamoja na usimamizi wa karibu, zana hizi huisaidia Benki Kuu ya Tanzania kupata matokeo ya ufanisi na na maendeleo katika sekta ya huduma za kifedha.

Sheria na kanuni za benki ni sehemu ya sheria na kanuni za serikali ambazo zinazitaka benki kutimiza masharti fulani, kuweka vizuizi na miongozo ili kujenga mazingira ya uwazi katika soko miongoni mwa taasisi za kibenki na watu binafsi and mashirika ambayo benki hizo zinafanya nayo kazi (ili kuendeleza sifa njema ya mfumo wa fedha nchini).

Mamlaka ya benki yanatokana na nyaraka ambazo ziko katika miundo ya sheria, kanuni, nyaraka  na miongozo.