Wakaguzi wa nje walioidhinishwa

Kwa mujibu wa Kanuni za Mabenki na Taasisi za Fedha (Wakaguzi wa Hesabu wa Nje), 2014, kampuni ya ukaguzi wa hesabu inayotaka kukagua benki au taasisi ya fedha inayofanya kazi Tanzania, lazima iombe kusajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania kama kampuni ya ukaguzi ya nje iliyoidhinishwa.

Kusajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania      
Zifuatazo ni hatua za kufuata ili kusajiliwa kama mkaguzi wa hesabu wa benki na taasisi za fedha zinazofanya kazi nchini, na ambazo zinasimamiwa na Kanuni za Mabenki na Taasisi za Fedha (Wakaguzi wa Hesabu wa Nje), 2014: -

    • Kila kampuni ya ukaguzi wa mahesabu inayotaka kuidhinishwa kama Mkaguzi wa Nje itawasilisha barua ya maombi Benki Kuu pamoja na: -
    • Maelezo ya kina ya muundo wa taasisi, makao makuu ya shughuli zake na matawi, na wka taasisi za ukaguzi wa hesabu za kimataifa, zitaeleza makao makuu yao pamoja masuala kisheria na kitaalamu ya kampuni mama;
    • Maelezo na sifa za wenye kampuni na watendaji wakuu zikionyesha uzoefu wao katika kukagua hesabu za benki na taasisi za fedha;
    • Orodha ya kazi kubwa za ukaguzi ambazo zimefanywa katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita na tozo zilizopokelewa kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita katika kila kazi ya ukaguzi iliyofanyika;
    • Uthibitisho kwamba kampuni ina angalau wafanyakazi wa kudumu 10 were elimu na uzoefu katika uhasibu na ukaguzi wa mahesabu, na angalau wanne kati yao wawe wamesajiliwa na Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu ya Tanzania (NBAA);
    • Maelezo ya kina ya uhusiano wowote ama wa moja kwa moja au usio wa moja kwa moja kati ya kampuni au mmiliki na benki au taasisi ya fedha yoyote;
    • Maelezo ya kina ya kampuni ambayo kuna makubaliano yoyote kuhusu ukaguzi
    • Taarifa nyingine yoyote ambayo Benki Kuu itaihitaji..

    For a list of approved external auditors bofya hapa